MASHEHA WAMETAKIWA KUJUA HAKI NA WAJIBU WAO KWA WANANCHI

TUME YA HAKI ZA BINADAMU

Tume ya Haki  za Binadamu na Utawala bora Tanzania imeendelea kutoa Mafunzo kwa Masheha wa Wilaya ya Mjini  yatakayowasadia katika kuwajengea uwelewa   wa kusimamia majukumu ya kazi zao za kuwahudumia Wananchi.

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa amewataka Masheha hao kusimamia vyema na watekelze Majukumu yao  kwa kujua nafasi ya haki za Binadamu na wajibu wao katika mazingira yao ya kazi na Jamii kwa ujumla na kufuata misingi ya haki, Kanuni na Utawala bora katika Jamii.

Katibu Msaidizi Tume ya haki na utawala bora Zanzibar Juma Msafiri Karibona amesema, wameamua kutoa Mafunzo hayo ilikuwawezesha kutambua Misingi na haki za Utawala bora na kuhakikisha masheha wanajua majukumu yao 

Wakizungumza Masheha walioshiriki katika Mafunzo hayo wameahidi kutekeleza na kuzingatia na kushauri tume ya haki za Binadamu kuzidi kutoa Elimu ya haki za Binadamu kwa Jamii na kuandaaa mpango Rasmi kwa kutoa Elimu kwa Wananchi ili kutambua haki na wajibu wao

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.