Akizungumza katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi ujenzi wa Hoteli ya Zanzibar Crown Resort, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema hatua hiyo itasaidia kukuza uchumi unaotokana na miradi hiyo kutokana na mahitaji ya Dunia, kubadilika na kufanya kazi kisasa mamlaka hiyo imekuwa ikiharakisha utowaji huduma na kuziomba Taasisi nyengine kujifunza kutoka kwao.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga, amesema mazingira bora ya uwekezaji na biashara pamoja na kufanya mageuzi ndani ya mamlaka ya kukuza uwekezaji, imechangia kumudu ushindani na Visiwa vyengine Duniani juu ya kuwepo miradi mikubwa.
Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar Sharif Ali Sharif, amesema wamepata mafanikio ikiwemo mikakati yake ya kuifungua Pemba kiuchumi pamoja na Uwekezaji wa Daraja la juu.
Zaidi ya shilingi bilioni 50 zitatumika hadi kumalizika kwa ujenzi wa Hoteli hiyo ambayo itatoa ajira zaidi ya mia mbili.