WIZARA YA AFYA INAWATAKA WANANCHI KUIMARISHA USAFI KATIKA MAENEO YAO ILI KUJIKINGA NA MALARIA

WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR

Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui ametakiwa Wananchi kuimarisha usafi katika maeneo yao ili kujikinga na maradhi mbali mbali ikiwemo Malaria.

Ametoa wito alipofanya ziara ya kukagua Majaa yameyoonekana kurundikana kwa uchafu na mazalio mengi ya Mbu katika maeneo mbali mbali ya Mkoa wa Mjini Magharibi amesema kutokana na kuongezeka kwa Maradhi mbali mbali ikiwemo Maradhi ya miripuko, Malaria na kuharisha kitengo cha afya ya mazingira imeona ipo haja ya kufanya ziara hiyo katika maeneo hayo ili kuweza kupata suluhisho ya kuondoa tatizo hilo.

Naibu Mkurugenzi kinga na elimu ya afya zanzibar Dkt Fatma Kabole amesema kutokana na kuwepo na ongozeko la Malaria hali ya Mazingira katika maeneo ya Jiji la Zanzibar hairidhishi hivyo amewataka Wananchi kuzidi kuimarisha usafi katika maeneo yao ili kuondokana na Maradhi.

Mkuu wa Kitengo cha elimu ya afya Zanzibar Bakari Hamad Magarawa na Mkuu wa kitengo cha afya ya mazingira wameahidi kuendelea kutoa elimu katika kupambana na Malaria na maradhi mbali mbali ya miripuko.

Ziara hiyo imefanyika katika maeneo ya Mji Mkongwe, Magofu ya Hoteli ya Bwawani na majaa mbali mbali ya Mkoa wa Mijini Magharibi.

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.