Ameyasema hayo huko Maziwang'ombe Wilaya ya Michweni Mkoa wa Kaskazini Pemba katika uwekaji wa jiwe la msingi la Skuli ya msingi ya ghorofa ya Maziwang'ombe ikiwa ni Shamra Shamra za maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Mheshimiwa Rais amesema serikali itaendelea kujenga Skuli za ghorofa katika kila eneo la visiwa ili kuwawekea Wanafunzi mazingira bora ya kusomea pamoja na kushughulikia changamoto za kimaslahi kwa Walimu.
Wakati huo huo Mheshimiwa Rais Mwinyi ameahidi kuwaajiri Walimu 1500 ili kuzidisha kasi ya upatikanaji wa Elimu nchini.
Awali Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Khamis Abdalla Said amesema ujenzi huo wa ghorofa tatu zenye vyumba 41 utaondoa changamoto ya msongamano wa Wanafunzi unao wakabili hivi sasa .
Nae Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mheshimiwa Salama Mbarouk Khatibu, amesema kwa kushirikana na wadau wengine wataendelea kusimamia shughuli zote za maendeleo katika Mkoa huo ikiwemo ujenzi wa majengo hayo ya Elimu.