Ameyasema hayo kwenye hafla ya uzinduzi wa Hoteli ya Ycona Luxury Resort huko Uroa Pongwe, amesema mafanikio ya kiuchumi yaliyofikiwa hadi sasa yametokana na amani na utulivu iliopo nchini.
Hivyo amesema kutokana na kuwepo fursa zaidi za kiuchumi ni vyema kuiunga mkono Serikali katika kufikia dhamira hiyo na ameipongeza ZIPA kwa mkakati wa kubuni miradi ya aina hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi ,Uchumi na Uwekezaji Mh. Mudrik Ramadhan Soraga amempongeza muwekezaji huyo kuwekeza katika utalii wa kimazingira ambao utasaidia kuondoa athari kwa wananchi wa maeneo hayo.
Akizungumza kwa niaba ya Muekezaji wa mradi huo Emanuel Johnson amesema mashirikiano waliyo oneshwa na wanakijiji yamemsaidia muekezaji huyo kubuni mradi mbadala, ikiwemo kuhifadhi Samaki baada ya kuvua.
Nae Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar ZIPA, Sharif Ali Shariff amesema Hoteli ya Ycona iliyohusisha majengo mbali mbali ikiwemo Mikahawa na Vyumba vipatavyo 40, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya kuwekeza miradi yenye hadhi ya juu.