Mshambulizi wa Paris St-Germain Kylian Mbappe anasema hajafanya uamuzi kuhusu mustakabali wake wa kuondoka au kubaki PSG.
Mkataba wa nahodha huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 25 na mabingwa hao wa Ligue 1 unamalizika msimu wa joto na amekuwa akihusishwa pakubwa na kuhamia Real Madrid.
Mbappe aliiambia PSG mwezi Juni kwamba hatachukua chaguo kwa miezi 12 zaidi katika mkataba wake.
Akizungumza baada ya kuifungia PSG wakiichapa Toulouse mabao 2-0 na kutwaa taji la Mabingwa wa Ufaransa.
alisema "Kama nilivyosema, tuna mataji ya kufuatiwa na tayari tumeshinda moja, hivyo hilo tayari limefanyika. Baada ya hapo. , hapana, sijafanya uamuzi bado.
Mbappe alijiunga na PSG mwaka wa 2017, awali kwa mkopo kutoka Monaco kabla ya uhamisho wa euro 180m (£165.7m).
Alikuwa anatazamiwa kuondoka kwa uhamisho wa bure mwishoni mwa msimu wa 2021-22 lakini hatimaye alitia saini nyongeza ya mkataba wa miaka miwili, na chaguo la mwaka zaidi.
Hata hivyo, baada ya Mbappe kuiambia PSG kwamba hatakubali nyongeza ya miezi 12 ya mkataba huo, hakuchaguliwa katika ziara yao ya kujiandaa na msimu mpya nchini Japan majira ya kiangazi.
Baadaye alikataa kukutana na wawakilishi wa klabu ya Saudi Pro League Al-Hilal, ambao walitoa ofa ya rekodi ya dunia ya £259m kwa ajili yake.
Mshambulizi huyo baadaye alirejea kwenye mazoezi ya kikosi cha kwanza kufuatia kile PSG walisema ni mazungumzo "ya kujenga.
Mbappe alikataa kuhamia Real Madrid alipokubali mkataba wake wa sasa na PSG mnamo Mei 2022 lakini huenda asiachie uamuzi kuhusu mipango yake mwishoni mwa wakati huu.
Wakati huo huo, mkufunzi wa Barcelona Xavi amesema kuwa wachezaji kama Mbappe hawawezi kufikiwa na klabu hiyo ya Catalan kwa sababu ya hali yao ya kifedha.