Akizungumza katika kazi ya uhakiki wa Wastaafu wanaolipwa Pencheni zao na mfuko huo katika uhakiki uliofanyika Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja na Mkoa w aMjini Magharibi, Mkuu wa Kitengo cha uhusiano ZSSF Raya Hamdani Khamis amesema mfumo huo mpya utaanza kutumika Mwezi julai mwaka huu ambapo Masheha wameshakabidhiwa Madaftari maalum ambayo yatahifadha taarifa za wastaafu.
Amesema kiasi ya Wastaafu elfu 13 na mia tano watafanyiwa uhakiki Unguja na Pemba kukiwa na ongezeko la Wastaafu ukilinganishwa na uhakiki uliofanyika mwezi Julai mwaka jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa ZSSF Nassor Shaban Ameir amesema kabla ya kuanza mfumo mpya ambao utakuwa wa kisasa watatoa elimu kwa masheha ili kuwarahisishia kazi hiyo.
Wastaafu hao wamesifu utaratibu mzuri wa uhakiki ambao umewaondoshea usumbufu.
ZSSF hufanya uhakiki kila baada ya miezi sita ili kufanya tasmini na kujua idadi halisi ya Wastaafu hao.