Akifungua Hospitali ya Wilaya ya kati Mwera Pongwe , Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla amesema kupitia ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025, Serikali imejenga Hospitali kumi za wilaya kwa Unguja na Pemba ambazo zina vifaa tiba pamoja na Gari za kubebea Wagonjwa.
Mh Hemed ameuagiza Uongozi wa Wizara ya Afya kuhakikisha Wanaisimamia vyema Hosptiali hiyo na Hospitali nyengine ili kufikia malengo yaliyokusudiwa na Serikali ya kuwapatia Wananchi huduma bora.
Mhe. Hemed amezitaka Kampuni ya Lancet na Saifee ambazo zimepewa Mkataba wa kutoa huduma Hospitalini hapo kuhakikisha huduma zote zinapatikana kwa wakati na kwa ubora wa hali ya juu kama makubaliano yanavyoelekeza.
Waziri wa afya Mhe Nassor Ahmed Mazurui amesema huduma za afya zimeimarika Zanzibar kwa kujengwa Hospitali za wilaya, Mikoa na Rufaa pamoja na kufanyiwa matengenezo makubwa baadhi ya Yituo vya Afya.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Amour Suleiman amesema jumla ya shilingi bilioni 9.7 zimetumika katika ujenzi wa mradi wa Hospital hiyo ambapo kwa wakati mmoja ina uwezo wa kulaza zaidi ya Wagonjwa mia moja na kupatiwa matibabu Hospitalini hapo.