Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.. Hussein Ali, Mwinyi amesema viongozi wanadhamira njema ya kuleta maendeleo endelevu yatakayo inua hali za uchumi kwa wananchi na huduma za jamii.
Dkt. Mwinyi amesema Serikali itaendelea Kuimarisha miundo mbinu kwa viwanja vya michezo kwa kuinua vipaji vya mazoezi ikiwemo kufanya mazoezi ili kuimarisha afya ya akili na kukuza uchumi kwa jamii ajira utalii
Akizungumza katika shamra shamra za kuadhimisha miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya mwaka 1964 katika mazoezi yalianzia mnarani, kisonge yalioishia uwanja wa amani amesema serikali imeamua, kuimarisha viwanja vya michezo ili kufanyika michezo mbali mbali.
Dkt.. Mwinyi ameitaka jamii kushiriki katika vikundi mbali mbali vya mazoezi, ili kuepukana na magonjwa mbali mbali na yasioambukiza, amesema ni jukumu la kila mmoja kulinda viwanja kwa maslahi ya nchi.
Ameipongeza ZADESA kwa jambo la kuweka mazingira safi na kutimiza azma ya siku ya usafi duniani na kuahidi Serikali itaunga mkono jitihada zao.
Amesema hili ni jambo la kuingwa na wananchi wote Serikali itashirikiana, ili kuleta mazingira bora amewataka wanchi kufanya mazoezi ili kuweka afya bora katika mazingira yao .
Waziri wa Habari Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Mh. Tabia Maulid, Mwita ametoa shukrani kwa Mh. Rais kwa kushiriki pamoja katika mazoezi, hayo ambapo amefanya mambo mengi katika michezo kwani yote hayo yametokanana na busara za viongozi.
Akisoma risala ya wanamazoezi ZABESA nd. Aviwa Juma amesema, Lengo ni kuhamasisha wananchi ili kuepuka maradhi na kutoa pongezi kwa mama mariam kwa kuhamasisha mazoezi tanzania.
Jumla ya Vikundi Mia Moja Na Hamsini 150 vimeshiriki Katika, Mazoezi Hayo ambayo yameanzia Muembe Kisonge, Michenzani yakiongozwa na Rais Dkt.. Hussein Ali Mwinyi, Viongozi mbali mbali na Wananchi, na kudhaminiwa na Benki ya NMB.