Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itaendelea kuimarisha ushirikiano na Serikali ya China ili kuchochea Maendeleo katika Sekta ya Uchumi, Elimu na Utamaduni.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Mhe.Shaaban Ali Othman wakati Akizindua Jumuiya ya Wazanzibar Waliosoma China OZACA huko kwenye Ukumbi wa Ofisi ya Ubalozi Mdogo wa China Mazizini
Amesema kuwa ushirikiano huo utaleta mabadiliko yatakayoibua fursa za Uwekezaji ambazo zitaendelea kukuza Maendeleo ya Taifa.
Balozi wa China Nchini Tanzania Zheng Ming amesema OZACA itasaidia kuunganisha Umoja kati ya China na Zanzibar kwa Maendeleo ya sasa na baadae na amewashauri Wanafunzi kuzitumia vizur fursa hizo za ufadhili wa Masomo.
Mwanzilishi wa Jumuiya ya Wazanzibar waliosoma China OZACA Maryam Khalfan amesema malengo ya Jumuiya hiyo ni kuchukua Wanafunzi Zaidi 80 kwa kwa Mwaka 2024-2025 hivyo ni vyema Wanafunzi kuzitumia fursa hizo za Elimu.
Sabrina Omar Abdalla ni miongoni mwa Wazanzibar Waliohitimu Nchini China amewashauri Wanafunzi kujiunga na Vyuo vya China kupitia fursa mbalimbli zilizopo kwa lengo la kuongeza ujuzi na kuleta Maendeleo ya Kielimumu Nchini.