DKT.MWINYI ASHUHUDIA UZINDUZI WA USAFIRI SGR

DKT.MWINYI

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi na Mke wake Mama Mariam Mwinyi wamehudhuria Uzinduzi wa Usafiri wa Treni ya Umeme kwa kutumia Reli ya Kisasa Standard Gauge Railway (SGR) wakitokea Jijini Dar es salaam hadi Dodoma. 

     Mradi huo wa kimkakati umezinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye pia alianza safari akitokea Dar es salaam kupitia Morogoro na kuwasili Dodoma. 

     Vilevile katika safari hiyo Rais Dk. Mwinyi alipata fursa ya kusalimiana na Viongozi mbalimbali ndani ya Treni hiyo wa Serikali, CCM, Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Mabalozi wanaoziwakilisha Nchi zao Tanzania, Vyombo vya ulinzi na usalama na Viongozi wa Dini pamoja na Wananchi

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.