Kiasi cha fedha Shilingi Trilioni 10 zimetumika katika ujenzi wa Reli ya Mwendokasi (SGR )kwa vipande vya kutoka Dar Es Salaam hadi Dodoma ikiwa dhamira ya Serikali ni kutanua Wigo wa kibiashara ambapo Reli hiyo inatarajiwa kufika hadi Nchi za Burundi na Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema hayo katika uzinduzi reli hiyo kutoka Dar es salaam, Morogoro hadi dodoma kwenye Kituo cha morogoro ambapo amewataka Wakulima kutumia fursa ya kulima Mazao mbalimbali na kupeleka katika Nchi ambazo zitafikiwa na reli ya mwendokasi.
Katibu Mkuu wa CCM Dkt Emmanuel Nchimbi ameongeza kuwa Watanzania wanajivunia mafanikio ya Uongozi wa Dkt Samia kwa kufanikisha kukamilika kwa Reli ya mwendokasi kwa zaidi ya km 1522 ambapo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adamu Malima amesema Morogoro ni sehemu ya ushahidi wa mafanikio ya Reli ya Mwendokasi.
Wananchi wa Mkoa wa Morogoro wameshukuru Serikali kuendelea kuleta maendeleo hivyo wameahidi kutumia fursa zilizopo ili kuzidi kunufaisha Mkoa.
Rais Samia atakuwa Mkoani Morogoro kwa ziara ya kikazi kuanzia agosti 2 hadi Agosti 7 ambapo atatembelea Miradi 14 ya sekta mbalimbali katika Wilaya za Morogoro.