WALIMU WAMETAKIWA KUUTUMIA MTAALA MPYA ILI KUONGEZA UFAULU

WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI

Wizara ya ELimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imewataka Walimu wa Skuli zote kuufuata Mtaala mpya wa Elimu ikiwemo kuwasomesha Wanafunzi Vitabu ili kuvifahamu, kufauli vizuri mitihani pamoja na kuwa na kuelewa wa Stadi za maisha.

Waziri wa Elimu Mhe Lela Muhamed Mussa akizungumza na Walimu katika Ziara ya kuangalia utekelezaji wa Mtaala mpya masomo kwa Skuli za msingi Mkoa wa kaskazini Unguja unavyotumika amesema Walimu wanawajibu wa kuhakikisha wanawasomesha Wanafunzi ipasavyo kupitia mtaala huo kufanya hivyo kutawajenga Wanafunzi kuwa Viongozo bora pamoja na kuelewa Stadi za Maisha na kuweza kujiari wenyewe wanapomaliza masomo.

Mkurugenzi idara ya Elimu za Maandalizi na Msingi Fatma Moode Ramadhani amewapongeza Walimu kwa kuutumia vizuri mtaala  huo katika ufundishaji jambo litakalopelekea kuongezeka kwa  ufaulu.

Walimu wa Skuli wa Mkoa huo wameahiidi kuendeleza kuutumia na kuitunza vyema mtaala huo ili Wanafunzi  waweze kufanya vizuri katika masomo yao huku wakiomba Wizara ya Elimu kuwatatulia matatizo wanayopitia ikiwemo uhaba wa Walimu na vitendea kazi. 

Waziri Lela amezitembela Skuli Tatu zikiwemo Skuli ya kidagoni mlimboni Kijini na Skuli ya Maandalizi na Msingi Kijini.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.