Kamati ya Skuli ya Msingi Uzini imeiomba Serikali kutengeneza Miundombinu ya Skuli hiyo kutokana na kuchakaa jambo linalosababisha usumbufu kwa Wanafunzi wakati wa kusoma.
Akizungumza katika ziara ya kukagua Skuli hiyo Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Ali Abdul-Gulam Hussein ambapo amesema uchakavu wa Miundombinu hiyo imekuwa tatizo la muda mrefu hali inayosababisha kutokupata huduma za msingi inayohatarisha ubora wa kiwango cha Elimu.
Mbunge wa Jimbo la Uzini Mhe Khamis Hamza chilo ameeleza jitihada wanazozichukua kwa kushirikiana na Wananchi katika kuhakikisha Wanafunzi wanapata Elimu bora za Elimu.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Ali Abdul-Gulam Hussein akitolea ufafanuzi mipango ya Serikali katika Ziara hiyo ameahidi kufanya matengenezo ya Skuli ya msingi uzini ili kuweka Mazingira Wezeshi ya kujifunzia yatakayoleta Tija kwa Wanafunzi.