ZAIDI YA AJIRA ELFU SABA KUPATIKANA KUTOKANA NA UWEKEZAJI WA VISIWA

Rais Dkt.Mwinyi

      Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema uamuzi wa kukodisha visiwa kwa uwekezaji wa muda mrefu ulikuwa uamuzi wa kimkakati ambao na kusababisha kusajiliwa kwa miradi 16 yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 384 za uwekezaji mtaji na kutoa ajira zaidi ya 7,000 kwa wenyeji.

      Rais Dkt.Mwinyi aliyasema hayo tarehe 11 Juni 2024, alipofungua Jukwaa la Uwekezaji na Uhifadhi wa Bahari Zanzibar katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Airport, Mkoa wa Mjini Magharibi.

     Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amesema dira ya maendeleo ya Zanzibar 2020-2050 inatambua uchumi wa buluu kama eneo la kipaumbele kwa kuleta maendeleo ili kuchochea mabadiliko ya kiuchumi kwa matumizi ya rasimali za bahari katika sekta ya uwekezaji.

     Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa ushirikiano kati ya Taasisi ya USAID Heshimu Bahari na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni mfano unaohitajika kuimarishwa na kukuzwa.

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.