Baada ya Majaribio ya Kuzalisha Sukari Mwaka Jana katika Kiwanda cha Sukari Mkulazi kilichopo Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro, Kiwanda hicho kwa sasa kimeanza rasmi uzalishaji wa Sukari Julai Mosi Mwaka huu ambapo mpaka sasa Tani zaidi ya Miatatu zimezalishwa na kuanza kuingia Sokoni.
Hayo yamebainishwa na Meneja wa Kiwanda cha Sukari Mkulazi Mhandisi Aron Mwaigaga mara baada ya Kamati ya Usalama Wilaya Kilosa ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya hii Bwana Shaka Hamdu Shaka kufika na kujionea Uzalishaji huo ulivyoanza.
Aidha akizungumzia namna Kiwanda hicho kinazalisha Umeme chenyewe kisha kuiuzia Tanesco Meneja wa Kiwanda cha Sukari Mkulazi Mhandisi Aron Mwaigaga amefafanua kuwa kwa sasa Kiwanda hicho kinatumia Umeme wake wenyewe huku Mtendaji Mkuu wa Kiwanda hiki Selestini Some Naye akieleza kuwa kwa sasa shughuli ya uzalishaji imeshaanza rasmi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilosa b Shaka Hamdu Shaka amesema Kiwanda hiki kitasaidia kuongeza upatikanaji wa Sukari ya Uhakika kwa