Waziri wa Afya Zanzibar Mhe.Nassor Ahmed Mazrui amesema kwa sasa Zanzibar imefanikiwa kuwafanyia upasuaji Watoto na Watu Wazima wenye Midomo wazi kwa awamu tofauti.
Amesema katika hatua hiyo iliyofikiwa Wizara itaendelea kushirikiana na Taasisi mbali mbali hasa The same Qualities katika kuimarisha afya za wenye matatizo ya Midomo wazi kwa kuwapatia matibabu kupitia Wataalamu hao na wanaotoka Nje ya Nchi.
Dkt. Samuel Siseja kutoka Taasisi ya The Same Qualities ya Arusha amesema Taasisi hiyo imeona kuna sababu za kushirikiana na Wizara ya Afya Zanzibar kuwafanyia upasuaji wenye tatizo hilo ili kuwarejeshea furaha yao na kuahidi kuendeleza ushirikiano huo.
stories
standard