DKT. SAMIA AWAHIMIZA WATENDAJI KUWAJIBIKA

DKT SAMIA SULUHU HASSAN
English

Raisi Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Amewaapisha Viongozi Aliowateua Hivi Karibuni Na Kuwataka Kuwajibika Ipasavyo Ili Kufanikisha Utekelezaji Wa Dira Ya Taifa.

Hafla Hiyo Ya Uapisho Iliyofanyika Ikulu Ya Magogoni Jijini Dar Es Salaam, Iliwahusisha Wakuu Wa Mikoa, Makatibu Wakuu, Makatibu Tawala Wa Mikoa, Naibu Makatibu Wakuu, Katibu Mtendaji Wa Tume Ya Mipango, Naibu Katibu Mtendaji Wa Tume Ya Mipango, Na Balozi Iliambatana Na Kiapo Cha Ahadi Ya Uadilifu Wa Watumishi Wa Umma.

Mara Baada Ya Kiapo Raisi Samia Anawakumbusha Makatibu Wa Kisekta Kila Mmoja Kwa Nafasi Yake Kubadilika Na Kuendana Na Kasi Na Matarajio Ya Wananchi Kulingana Na Sera Na Sheria Zilizopo, Huku Akitaka Tanzania Kujitegemea Katika Uzalishaji Wa Dawa Kwa Zaidi Ya Asilimia 70 Ifikapo 2030.

Dkt. Samia Amezitaja Sekta Za Kilimo, Mifugo Na Uvuvi Kuwa Ni Sekta Ambazo Mavuno Yake Yanahitajika Hivyo Amesisitiza Kusimamiwa Kisayansi Ili Ziweze Kuleta Tija Kwa Kuwainua Vijana Na Kuleta Mapato Kwa Taifa.

Kwa Upande Wa Wakuu Wa Mikoa Ya Mtwara Na Kagera, Wamekumbushwa Umuhimu Wa Mikoa Yao Ambayo Ni Ya Kimkakati Na Kusisitizwa Kuimarisha Ulinzi Na Usalama Katika Maeneo Yao.

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.