Kiongozi wa Timu ya 33 ya Madaktari kutoka China Dkt.Jiao Cheng amesema wataendelea kushirikiana na Madakatari wa Upasuaji Nchini Tanzania kwa kupeana taalamu kwa lengo la kutoa huduma ubora kwa Wananchi.
Akizungumza katika Mkutano wa 29 wa Chama cha Madaktari wa Upasuaji Tanzania uliofanyika Mkoani Morogoro ambao umewashirikisha Madaktari mbali mbali wa Upasuaji Nchini, Dkt.Jiao amesema Mkutano huo unawezesha kupeana utaalamu zaidi katika huduma za Upasuaji.
Akiwasilisha Mada ya juu ya upasuaji wa kutumia Matundu madogo Dkt.Jiao amesema njia hiyo ni ya kisasa na rahisi na inamuwezesha Mgonjwa kupona haraka.
Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari wa Upasuaji Dkt.Baiya Abdallah Rashid amewataka Madaktari Chipukizi wa Upasuaji kujiunga na Chama hicho ili kupata fursa za kujifunza na kubadilishana uzoefu.
Hata hivyo amewaasa Madaktari wa Upasuaji kufanya tafiti ili kuweza kubaini Magonjwa yanayowakabili Binadamu.
Malengo ya Mkutano huo ni kujadili jinsi ya kusogeza huduma za Upasuaji karibu na Jamii kupitia Kambi zinazoandaliwa kupitia Chama hicho.