Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mh Mudriq Ramadhan Soraga amesema huduma za Msingi za Kijamii ni muhimu ziwepo katika maeneo ya Miji mipya kwani Serikali inaendelea kutoa msisitizo kwa wawekezaji kuweka huduma za Kimtandao katika maeneo hayo.
Akizungumza na Wadau wa uwekezaji wa Ujenzi wa Miji Mipya na Maendeleo ya Kiuchumi Zanzibar huko Fumba Town amesema Sekta ya Ujenzi ya Nyumba za Makazi inakuwa kwa haraka kwani imetoa Vivutio vikubwa ambapo Wawekezaji wanajitokeza.
Aidha amefahamisha kuwa Afrika School Ikonomic itawekeza katika maeneo ya Fumba na Miradi mengine hivyo amewaomba Wawekezaji hao kuwashirikisha Wananchi katika Miradi hiyo ikiwemo Ajira.
Kwa upande wao Wawekezaji hao wameahidi kufuata maelekezo ya Serikali na kuomba ushirikiano na Wananchi ili kufanikisha Malengo ya Miji mipya.