Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ya Zanzibar ina Mpango wa kuzigeuza Taka kuwa MAli ghafi inayoweza kutumika tena ikiwemo kutengeneza Mbolea.
Akijibu suali katika Kikao cha Baraza la Wawakilishi Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na idara maalum za SMZ Mhe Masoud Ali Mohamed amesema Wizara kupitia Halmashauri na Mabaraza ya Miji, zimekuwa zikitoa Mafunzo kwa ajili ya kuwawezesha Wananchi kuweza kuzisarifu Taka hizo.
Hata hivyo amesema wamekuwa wakifanya ukaguzi katika Hotel za Kitalii na kuwaomba kuzitenganisha Taka hatarishi na Taka za kawaida kabla ya kuziondoa katika maeneo yao husika
Wakati huo huo Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, imesema haitoi Vyeti kwa wanafunzi waliomaliza Darasa la Saba, ambao wamepata fursa za Masomo nje ya Nchi
akijibu suali katika Kikao cha Baraza la Wawakilishi naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe Ali Abdulgulam hussei amesema kwa sasa Vyeti ambavyo watoa ni kwa Wanafunzi ambao wamemaliza Kidato cha Nne, ambao ndio wanaotambuliwa kuwa wamemaliza Elimu ya lazima kwa mujibu wa Sera ya Elimu.