Naibu Waziri Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amalii Mhe.Ali Abdulgulam Hussein amesema kujengewa uwezo Walimu kutasaidia kufikia malengo ya Serikali katika kuimarisha elimu Nchini.
Akifunga Mafunzo kwa Walimu na Wasaidizi Walimu Wakuu wa Skuli za Mkoa wa Kusini na Kaskazini Unguja huko Kituo cha Ubunifu Jangombe Naibu Waziri amesema kuwa Serikali itaendelea kuimarisha mazingira bora ya Walimu na kuwapatia Mafunzo Kazini ili kufanyakazi kwa ufanisi.
Amesema Wizara kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo Wataendeleza juhudi za kuwapatia ujuzi Watendaji wake kusudi kuendana na mabadiliko katika Elimu.
Akitoa Muhutasari wa Mafunzo waliyopatiwa Walimu hao Meneja Mwandamizi Goodneibor John Maseza amesema Walimu zaidi ya 500 wamepatiwa Mafunzo ya Uongozi na Usimamizi wa Skuli ili kuweza kumudu kutekeleza majukumu yao.
Masenza amesema Mafunzo hayo ni mwendelezo wa lengo la kuwajengea ujuzi Walimu ikiwa ni utekelezaji mpango Mkakati wa ufundishaji kwa umahiri.
Nao Wahitimu wa Mafunzo hao yaliyokuwa ya Siku Sita wameahidi kwenda kuyatekeleza kwa Vitendo ili malengo ya Serikali yafikiwe.