Jumuiya ya Watu Wanaoishi na Maradhi ya Sikocell imeitaka Jamii kutowatenga Watu Wanaoishi na Maradhi hayo kwani ni sawa na mengine.
Akizungumza kwa Nyakati tofauti katika kutoa elimu kwa Ugonjwa wa Sikocell kwa Wanafunzi na Walimu wa Skuli ya Dr.Ali Muhammed Shein na Haile Salasi Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Damu kutoka Hospital ya Mnazi Moja Dkt.Thuwein Nasor Said amesema hali hiyo itaongeza mapenzi baina yao.
Akitaja dalili za Ugonjwa huo ikia ni miongoni ukuaji wake dhaifu, upungufu wa Damu kutoweza kula pamoja na kubadilika kwa rangi na kuwa njano.
Miongoni mwa Watu ambao wanaishi na mardhi hayo wamewasihi Watu wengine kutowambia Maneno ya yanayoashiria unyanyapaa kitendo ambacho hakikubaliki katika Jamii.
Walimu na Wanafunzi waliopatiwa Elimu hiyo wameishukuru Jumuiya Seli Nyekundu au Sikocell kwa kuwapatia Elimu hiyo na kuahidi kuifikisha ili lengo liweze kufikiwa.
Siku ya Ugonjwa huo huadhimishwa kila ifikapo Juni 19 ambapo kwa hapa Tanzania zaidi ya Watoto Kumi na Moja Elfu Huzaliwa na Ugonjwa huo wa Sikocell kila Mwaka .