Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mh.Lela Mohammed Mussa amewaomba Wamiliki wa Skuli Binafsi kukaa pamoja na Wazazi kwa ajili ya ulipaji Ada ya Masomo pindi Mwanafunzi anapochelewa kulipiwa Ada hiyo.
Akizindua huduma ya Lipa Ada kwa Skuli Binafsi Waziri Lela amesema huo ni ubunifu wa Teknolojia ambao utarahisisha kutumika utendaji katika Sekta ya Elimu.
Amesema suala la kulipa Ada ni la Mzazi na sio Mwanafunzi hivyo si vyema kuwanyanyasa Wanafunzi ikiwemo kuwatoa Madarasani wanapochelewa kulipiwa Ada hiyo.
Afisa Mkuu Tigo Pesa Angelica Pesha amesema Mfumo huo utaondoa usumbufu kwa Wazazi na Walimu kupata suluhisho kwao na kuleta ufanisi katika Elimu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Zmotion Taasisi inayojishughulisha na Mifumo (Zmotion) Ndg.Said Hemed Ali amesema wameamua kuleta mfumo huo ili kuisaidia Serikali katika kufanya kazi Kidigitali