Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb.), ametembelea banda la maonesho la kampuni ya ZTE linaloonyesha mafanikio makubwa ya matumizi mbalimbali ya Akili Mnemba (AI) na Mtandao wa Vitu (IoT), katika kituo cha Kimataifa cha Mikutano Geneva, nchini Uswisi.
Waziri Nape alisema kuwa Akili Mnemba (AI) na Mtandao wa Vitu (IoT) ni teknolojia muhimu sana katika kuongeza uzalishaji na ufanisi. Hivyo teknolojia hizi zipewe kipaumbele ili kuwezesha watu kufanya kazi zenye kuleta matokeo chanya katika jamii.
Ameongeza kuwa uwepo wa teknolojia hizi ziwe chachu katika kuleta mabadiliko kwa kukuza na kuongeza ubunifu wa kufanyakazi mbalimbali na kuongeza ufanisi katika kazi pasipo kutegemea ajira.
“Ushauri wangu kwa makampuni makubwa kama ZTE kwa sababu teknolojia hizi zinaleta ongezeko la mapato hivyo sehemu ya mapato hayo ya ziada yangetumika kuwasaidia watakaopunguzwa kazini kuanza maisha mapya badala ya kuwaacha tu barabarani” -Waziri Nape.