Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Abdulurhaman Kinana amewataka Watanzania kushiriki katika Kampeni ya matumizi ya Nishati safi ya kupikia yenye lengo la kutokomeza matumizi ya Mkaa na Kuni ili kuhifadhi Mazingira
Makamo Kinana ametoa kauli hiyo akiwa Wilayani Morogoro Vijijini wakati Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki Hamis Taletale akitoa Taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi mkuu katika kipindi cha Miaka Mitatu sambamba na ugawaji Mitungi ya ya Gesi ya Oryx 800 yakiwa na Majiko yake kwa Wananchi wa Wilaya hiyo ambapo akatumia fursa hiyo kueleza dhamira ya Rais Samia katika kuhamasisha Nishati safi ya kupikia.
Kwa upande wake Meneja wa Mifumo ya Gesi yenye matumizi makubwa Oryx Gas Tanzania LTD, Richard sawere amesema ugawaji wa Mitungi hiyo ni kuunga mkono jitihada za Rais Dk. Samia ambaye amedhamiria ifikapo Mwaka 2030 Asilimia 80 ya Watanzania wawe wananatumia Nishati safi ya kupikia.
Awali Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki Hamis Taletale ameishukuru kampuni hiyo kwa kufanikisha ugawaji bure wa Mitungi hiyo kwa Wananchi zaidi ya 880 na lengo ni kumuunga Mkono rais Samia Suluhu Hassan.