Kampeni ya Msaada wa Kisheria inayoenda kwa Jina la “Mama Samia Legal Aid” imezinduliwa Rasmi Mkoani Njombe ambapo Wananchi wa Mkoa huo wametakiwa kuitumia vyema nafasi hiyo ili kukutana na Mawakili wabobevu watakao zunguka katika maeneo yao kwa ajili ya kutatua matatizo yanayowakabiri ikiwemo migogoro ya ardhi mirathi na ndoa.
Naibu Waziri Mkuu Dotto Biteko ndiye aliyekuwa Mgeni rasmi katika Hafla hii ya Uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa kisheria ameipongeza Wizara hiyo kwani kupitia Kampeni hii imeonyesha wazi uelewa kwa Wananchi umeongezeka kwani mpaka sasa Wanaume wanaongoza kujitokeza kupata msaada wa kisheria ikiwa zaidi ya Watu Laki Tano wamepata huduma hii huku Wanaume ikiwa ni 216000 na Wanawake ni 199000 wamejitokeza kupata msaada wa Kisheria.
Deodatus Mwanyika ni Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini amempongeza Serikali kwa kuanzisha Kampeni hii ya kusikiliza Kero za Wananchi mpaka Maeneo ya Vijijini ambapo amesema kuwa wao kama Wawakilishi wa Wananchi wanaamini kuwa changamoto ya migogoro miongoni mwa Wananchi itaenda kupungua.