Afisa Mdhamini Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Pemba, Mfamau Ali Mfamau amesema Viongozi wa Nchi wamekua wakiwekeza katika Viwanja vya Michezo kwa kujenga Viwanja vya Kisasa zaidi.
Mdhamini Mfamau ameyaleza hayo katika Hafla ya Uzinduzi wa Mradi wa Michezo na Maendeleo, unaotekelezwa na Kituo cha Majadiliano kwa Vijana Zanzibar (CYD kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Wizara ya Elimu na Wizara ya Maendeleo ya Jamii jinsi kwa ufadhili wa Shirika la Ujerumani (GIZ).
Amesema katika Kipindi hiki cha Ujio wa Afkon, kuna Viwanja vingi vinakuja kwa Michezo yote na Rais ataona Faraja watu kushiriki Michezo kwa Makundi yote.
Mratibu wa CYD Pemba Ali Shabana Mtwana, amesema lengo la CYD ni kuwasaidia Vijana katika nyanja tafauti, ambapo mradi wa michezo na maendeleo umekusudia kuwafikia Watu wengi.
Afisa Elimu Wilaya ya Chake Chake Burhan Khamis Juna na baadhi ya Wadau wa Michezo waliohudhuria Uzindizi wa mradi huo walikua na haya ya kueleza.