Watanzania leo wamefanya kumbukizi ya Miaka 28 ya Ajali ya Meli ya Mv. Bukoba iliyotokea Mwaka 1996 katika Ziwa Victoria, huku baadhi ya Wananchi waliopoteza Ndugu na Jamaa zao katika ajali hiyo wakiiomba Serikali kuienzi Siku hiyo na kuimarisha usalama wa Vyombo vya Majini.
Kumbukizi hiyo imefanyika katika Makaburi ya baadhi ya Waliofariki katika Ajali ya Mv. Bukoba yaliyopo Igoma Jijini Mwanza.
Paroko wa Parokia ya Nyamhongolo Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza Padri George Nzugu ameongoza Sala ya kuwaombea Marehemu hao.
Wakazi wa Mkoa wa Kagera na Mwanza walioshiriki Kumbukizi hiyo wamesikitishwa na Mwitikio Mdogo wa Wananchi waliojitokeza ili kuwakumbuka Ndugu zao ikilinganishwa na hali ilivyokuwa Miaka ya Zamani.
Musa Ntobi ni Mwangalizi wa Makaburi ya waathiriwa wa Ajali ya Meli ya Mv.Bukoba ambaye anawahimiza Watanzania kuendelea kuienzi Kumbukizi hiyo.
Mkurugenzi Mkuu Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania Tasac, Mohamed Salum amesema ili kudhibiti Ajali za Majini ambazo zimekuwa zikigharimu Maisha ya Abiria na mali zao Wakala huo umeimarisha ukaguzi wa Vyombo vya Usafiri wa Majini.
Meli ya Mv.Bukoba imepata ajali ya kuzama Mei 21, Mwaka 1996 ikiwa inakaribia katika Bandari ya Mwanza Kaskazini ikitokea Bandari ya Bukoba kupitia Kemondo. inakadiriwa kuwa zaidi ya Watu Mia Tisa wamepoteza Maisha katika Ajali hiyo.