Mahkama Kuu Zanzibar imetiliana Saini na Ubalozi wa Nchini Tanzania Switzerland juu ya muongozo wa kutaifisha mali ambazo zimepatikana kwa njia ya uhalifu.
Akizungumza mara baada ya Utiaji Saini huo Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Khamis Ramadhan Abdallah amesema Utiaji Saini huo ni utaratibu wa kuzitaifisha mali ambazo zimepatikana kwa njia ya uhalifu na kuhakikisha Mhalifu halipwi kwa mujibu wa Sheria zilizopitiwa katika Mkataba huo miongoni mwa Sheria hizo ni Sheria za Dawa za Kulevya , mwenendo wa makosa ya Jinai na sheria za KMKM.
Balozi wa Switzerland Nchini Tanzania Didier Chassot amesema watashirikiana na Mahkama za Zanzibar katika kuzirejesha mali zilizotaifishwa kwa uhalifu na kuzirejesha Serikali kupitia muongozo huo.
stories
standard