Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais,Katiba,Sheria Utumishi na Utawala bora imesema Mwaka wa fedha 2024/2025 imepanga kutekeleza Bajet yake kwa kuzingatia vipaumbele vya kuendeleza Mifumo ya Kieletrpnic katika Utumushi wa Umma na kusimamia misingi ya Utawala bora.
Akiwasilisha Hutuba ya Makadirio ya Mapato ya Wizara hiyo Waziri wa Wizara hiyo Mh Haruna Ali Sleimain amesema kufanya hivyo kutasaidia Kuimarisha vipaumbele vyengine ikiwemo kusimamia misingi ya maadili, kuongeza mapambano zidi ya Rushwa pamoja na ukaguzi na udhibiti wa Rasilimali za Umma.
Waziri Haroun amesema ili kutekeleza Majukumu hayo Wizara hiyo imeomba kutengewa zaidi ya Shiling Bilioni Mia moja kwa Ajili ya Mishahara na Mtumizi mengine ya Ruzuku .
Mwenyekiti wa Kamati ya kuchungunguza Hesabu za Serikali ya Baraza la Wawakilishi PAC Mhe Juma Ali Khatibu amesema kamati imebaini kuwa baadhi ya Taasisi za Serikali hazifikii mapato ya ukusanyaji kutokana na usimamizi usioridhisha.
Mjumbe wa kamati ya kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu Kitaifa Mh Mariam Thani ameiomba Serikali katika Mwaka wa Fedha 2024/2025 Kamati hiyo kupatiwa Fedha za kutosha ili kutatua matatizo mbali mbali yanayowakabili katika shughuli zao za ufuatiliaji.