SUZA YATILIANA SAINI HATI YA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO NA CHUO CHA TAIFA CHA UTALII (NCT)

UTIAJI SAINI

      Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) kimetiliana Saini hati ya makubaliano ya ushirikiano na Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) wakilenga uimarishaji wa Sekta ya Elimu katika masuala ya Utalii na kukuza Sekta hiyo.

     Hafla ya Utiaji Saini ilifanyika katika Chuo cha Taifa cha Utalii Jijini Dar es salaam na kushuhudiwa na Makamo Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA Profesa Mohamed Makame Haji na Mkuu wa Chuo cha Utalii Dr. Florian Mtey hatua iliyotajwa kusaidia kuimarisha utoaji wa huduma za Utalii zenye viwango na kuchangia ongezeko la Watalii Nchini.

     Akizungumza katika hafla hio Makamo Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA Profesa Mohamed Makame Haji amesema Uchumi wa Buluu ni eneo ambalo linaimarika kwa Kiwango kikubwa kutokana na nguvu kubwa iliyowekwa na Viongozi Wakuu wa Taifa hili, hivyo imewalazimu kuwa na mikakati ya pamoja ili kwenda sambamba na kasi hiyo.

     Professa Mohamed ameongeza kuwa Taasisi za Elimu zina jukumu la kuangalia mahitaji halisi ya Jamii ikiwemo kuwajengea vijana uwezo na utaalamu wa kuwakirimu watalii wanaotembelea Nchini.

      Awali Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii NTC Dr. Florian Mtey ameyataja maeneo ya ushirikiano na kusisitiza juu ya umuhimu wa kuzalisha watoa huduma walio bora kwa mujibu wa Viwango vya Kimataifa.

     Sekta ya Utalii ni Sekta muhimu sana kwa Uchumi wa Taifa la Tanzania ambapo inatoa Mchango wa Asilimia 17.5 ya pato la Taifa na Asilimia 25 ya Fedha za Kigeni.     

            

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.