Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh.Lela Mohammed Mussa amesema Wizara hiyo itahakikisha inawatafutia Wanafunzi wenye fursa za kusoma Nchi mbalimbali ili kuona wanapata taaluma zitakazowasaidia katka kuleta maendelo ya Nchi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Mh.Lela amesema amepokea ujio wa Balozi wa Poland aliyekuja kwa lengo la mahusiano katika Sekta ya Elimu ya juu kwa Poland na Zanzibar ili Wanafunzi wa Zanzibar wapate ufadhili wa kusoma fani tofauti ambazo zinaenda na sayansi na teknolojia.
Mh.Lela pia amesema ongezeko la Watalii wengi wanaotoka Nchini Poland ndio sababu ya kupeleka Balozi huyo kuja kutaka makubaliano katika Sekta ya Elimu na wanataka wapate Ubalozi wao Zanzibar
Wanafunzi wa Zanzibar watahakikisha wanapata ufadhili wa masomo Nchini Polanda na kupata Maarifa yatakayokuza maendleo ya Nchi.