WANANCHI WAMETAKIWA KUPIMA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

MKURUGENZI MKUU WIZARA YA AFYA

Wanawake wenye umri kuanzia Miaka 18 hadi 69 wametakiwa kujitokeza kwenye upimaji wa Saratani ya shingo ya Kizazi katika Hospitali ya Mnazi Unguja Mmoja na Chakechake Kisiwani Pemba

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt Amour Mohamed Suleiman alipokuwa akizungumza na Timu ya Madaktari kutoka China wanaotarajiwa kuanza zoezi la upimaji wa Saratani ya shingo ya Kizazi hapa Zanzibar.

Amesema ni muhimu Wananchi kutumia fursa hii ya uchunguzi wa Saratani ya Shingo ya Kizazi,ili kuweza kubaini Ugonjwa kwenye hatua za Awali na kuepukana na athari hapo baadae.

Naibu Mkurugenzi Qi Xiaomin kutoka Nanjing Hospital  katika jimbo la Jiangsu Nchini China amesema kuwa wapo tayari kuendelea kuisadia Zanzibar kwenye upande wa Vifaa tiba na Mafunzo kwa Madaktari wazawa katika uchunguzi wa Saratani ya shingo ya Kizazi.

Uchunguzi wa Saratani ya Shingo ya Kizazi unatarajiwa kuanza tarehe 21 Mwezi huu na kukamilika Tarehe 19 Mwezi wa Sita Unguja na Pemba

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.