Jaji Dhamana wa Mahakama kuu Zanzibar,Kisiwani Pemba,Salim Hassan Bakari amewataka Maafisa Manunuzi,na Wahasibu kuwa waadilifu kwa kutojihusisha na Rushwa na badala yake kusimama imara katika kupiga vita vitendo hivyo kwenye utekelezaji wa majukumu yao.
Jaji Dhama ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Maafisa Manunuzi Wahasibu na Wanasheria katika hafla ya ufungaji wa Mafunzo ya Sheria za Manunuzi huko makatiba kuu ya Chake Chake.
Amesema katika sehemu ya Manunizi kumekuwa kukijitiokeza vishawishi vingi vya Rushwa na ufisadi katika kufanya manunuzi jambo linaloweza kuisababishia hasara Serikali hivyo aliwataka Maafisa hao kusimama imara katika kupiga vita adui huyo.
Aidha Jaji huyo aliwaomba Maafisa hayo kuangalia sheria ambazo zinakwanza katika utekelezaji wake ili ziweze kufanyikwa marekebisho.
Mapema Mratibu wa Mafunzo hayo amesema ni sehemu wa kuchochea uwajibikaji,uwazi na kuwajengea uwezo kwa kufanya kazi zao kwa weledi huku yakiwashirikisha Maafisa manunuzi Wahasibu na Wanasheria.
Mafunzo hayo ya Siku Saba yaliwashirikisha Maafisa Wahasibu na Wanasheria wa Taasisi mbali mbali za umma Kisiwani Pemba.