Wakaazi wa Jimbo la Magomeni wameomba kukamilishiwa Ujenzi wa Mitaro katika Maeneo yao pamoja na kuimarishiwa Miundombinu ya Maji ili kuwaondoshea kero Wananchi.
Wakaazi wa Jimbo hilo wakizungumza wakati Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Kichama Talib Ali Talib akiendelea na Ziara zake za kusikiliza kero za Wananchi, wamesema wamekuwa wakipata adha ya Nyumba zao kuingia maji wakati wa Mvua kutokana na kukosekana Mitaro pamoja na shida ya Maji.
Wakijibu malalamiko ya Wananchi, Mwenyekiti huyo wa Mkoa wa Mjini Kichama Talib Ali Talib na Diwani wa Wadi ya Magomeni Haji Ali Haji, wamewaelezea Wananchi jitihada zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali kuhakikisha maeneo yote yanaimarishwa Miundombinu ya Mitaro pamoja na upatikanaji wa Maji safi na salama.
Jimbo la Magomeni ni la Pili kutembelewa na Mwenyekiti huyo tokea alipoanzisha utaratibu wa kusikiliza Kero kwa Majimbo yote katika Mkoa wa Mjini Kichama.