SERIKALI YAJIPANGA KUIMARISHA HUDUMA YA MAJI SAFI KATIKA SKULI ILI KUWAKINGA WANAFUNZI NA MARADHI YA MRIPUKO

Waziri Lela

     Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ina mpango mkakati wa kuimarisha miundombinu ya maji safi na salama katika Skuli ili kuwakinga Wanafunzi na maradhi ya mripuko.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.  Lela Muhammad Mussa amesema kwa kushirikiana na Wadau, watahakikisha mazingira ya kuisoma katika Skuli yanenda pamoja na kuwepo huduma hiyo ya maji safi na salama ili kuimarisha ustawi wa Wanafunzi, Waziri Lela ametoa kauli hiyo wakati akifungua Mkutano wa Wadau 22 wa Kimataifa hapa Zanzibar.

      Afisa wa Shirika la kuhudumia Watoto Unicef Marko John Msambazi amesema katika Sekta ya maji na usafi wa mazingira wanaendelea kudumisha ubunifu katika Jamii ili kufahamu suala zima la usafi.

     Wakati huo huo Mhe.Lela amewatembelea Wanafunzi  wa Skuli ya Tumekuja wanaosoma kwa njia ya mtandao kutoka Kibaha kuona maendeleo ya Wanafunzi hao ili kujua maendeleo ya Masomo yao.

     Mkurugenzi Idara ya Teknolojia Habari na Mawasiliano katika Sekta ya Elimu Zanzibar Mbwana Yahya Mwinyi amesema kuanzishwa kwa mfumo huo utawawezesha Wanafunzi kupata Elimu yenye manufaa huku Wanafunzi wa Skuli hiyo wameishukuru Serikali kwa kuwaletea mfumo wa kushiriki masomo na Wenzao kupitia mtandao wa Kijamii na kupata ujuzi zaidi.

hot
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.