Wanafunzi na Walimu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA Idara ya Kompyuta na Mawasiliano ya Habari wamesema Waandishi wa Habari Wachanga Wana Wajibu wa kulinda misingi na ya Habari ili kuimarisha Amani Nchini.
Wakizungumza katika Ziara ya kujifunza kwa Vitendo huko Shirika la Utangazaji Zanzibar Mnazi Mmoja ikiwa ni Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani wamesema hatua hiyo itasaidia shughuli za Maendeleo kufanyika kwa utulivu.
Aidha wamesema kujifunza kwa vitendo kunasaidia kuongeza uzoefu na kujua njia bora ya utendaji katika Tasnia ya Habari.
Naye Mkurugenzi Rasilimali Watu wa Shirika la Utangazaji Zanzibar Ndg.Salum Suleiman Jecha amesema Ziara ya Wanafunzi hao inaonyesha ukubwa wa ZBC Nchini na kufahamisha kuwa Ziara hiyo itaongeza ufanisi kwa Wanafunzi hao.
Akizungumzia Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Mkurugenzi huyo amesema Waandishi wa Habari wana wajibu wa kujikita katika kufanya tafiti ili kuibua mambo mbalimbli ya maendeleo kwa Taifa .
Ziara ya Wanafunzi wa SUZA ina lengo la kuunga mkono Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani iliyoasisiwa Mwaka 1993 na Baraza la Kuu la Umoja wa Mataifa.