Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Mhe.Masoud Ali Mohammed, amesema Ujenzi wa Ofisi za Masheha katika Shehia itawawezesha kuongezeka uwajibikaji na Wananchi kuwa huru pindi wanapofata huduma.
Akitembelea Ujenzi wa Ofisi ya Sheha Shehia ya Ijitimai Mwanakwerekwe, amemtaka Mkandarasi wa Ujenzi huo Kikosi cha KVZ kuharakisha Ujenzi huo ili kuwawezesha Masheha kuongeza ufanisi wa kiutendaji kwa Wakaazi wao.
Mkuu wa Wilaya ya Magharib 'b', Hamida Mussa Khamis, amesema anamatarajio kwa Masheha kuleta mabadiliko na kuwaondoshea mazingira magumu ya kazi waliyokumbana nayo hapo kabla.
Mkandarasi wa Ujenzi huo Mkuu wa Kikosi cha Valantia KVZ, Luten Kanal Said Ali Shamhuna, amesema Ujenzi huo umezingatia kiwango cha ubora kinachosimamiwa na Wakala wa Majengo Zba na kuahidi kukamilika kwa wakati uliopangwa.
Nae Sheha wa Shehia ya Ijitimai Rashid Mwadini Omar, pamoja na Mwananchi wa Shehia hiyo wamepongeza hatua ya Serikali kuwajengea Ofisi ambazo zitaleta ufanisi na usiri wa kazi, tofauti na hapo awali.
Jumla ya Ofisi 388 zinatarajiwa kujengwa kwa kila Wilaya za Unguja na Pemba .