Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamad Khamis Hamad amesema Ushirikiano wa Kidiplomasia kati ya Tanzania na Nchi za Falme za Kiarabu kutatoa fursa za kubadilishana uzoefu baina ya pande mbili hizo na kuimarika kwa ulinzi katika Miradi ya maendeleo Nchini.
Akizungumza na Balozi mdogo wa Nchi za Falme za Kiarabu Mhe. Saleh Ahmed Alhemeiri, CP Hamad ameomba uwezekano wa kuongezewa taaluma kwa Askari wa Jeshi la Polisi kuhusiana na makosa ya Kimtandao makossa ambayo yamekuwa changamoto Duniani.
Balozi mdogo wa Nchi za Falme za Kiarabu Mhe. Saleh Ahmed Alhemeiri amesema ziara yake makao Makuu ya Polisi Zanzibar ni kuendeleza ushirikiano wa Kihistoria baina ya Tanzania na Nchi za Falme za Kiarabu na ameahidi kuimarisha ushirikiano wa Majeshi ya Polisi baina ya Tanzania na UAE.