DKT.MWINYI AHIMIZA WATOTO KUFUNDISHWA HISTORIA YA MUUNGANO

Dkt.Mwinyi

     Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema kuna wajibu wa kuwaenzi waasisi wetu kwa kuweka Kumbukumbu zao, pia amehimiza kufundisha watoto historia ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

      Rais Dk.Mwinyi amesema hayo wakati wa hafla ya utoaji nishani kwa viongozi mbalimbali na uzinduzi wa vitabu viwili cha Historia ya Ofisi ya Makamu wa Rais na safari ya picha ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni shamrashamra za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika viwanja vya Ikulu Chamwino tarehe: 24 Aprili 2024.

      Aidha Rais Dk.Mwinyi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kurudisha mashindano ya kombe la Muungano, amewakaribisha wananchi wote kushuhudia mashindano hayo .

     Vilevile Rais Dk.Mwinyi amempongeza Rais Dkt.Samia kwa kutendea haki shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar iliyoambatana na uzinduzi wa Kitabu cha historia ya Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na safari ya picha ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

      Halikadhalika Rais Dk.Mwinyi ameleeza kuwa viongozi wa pande mbili za Muungano wamefanya kazi kubwa ya kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo.

 

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.