Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, Dkt. Khalid Salum Mohamed amesema kuwa Barabara ya Tunguu, Makunduchi inatarajiwa kujenga hivi Karibuni.
Dkt. Khalid amesema hayo katika ziara ya kutembelea Barabara zilizoatharika kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha hapa Nchini.
Katika ziara hiyo pamoja na Viongezi wengine wa Wizara yake walitembelea Barabara ya Tunguu -Makunduchi, Kitogani, paje na Bwejuu katika Mkoa wa Kusini Unguja na kuona Barabara hizo zilivyoathirika.
Amesema Serikali imeandaa Mpango wa Dharura wa kufanya matengenezo Barabara hizo ili kuwarahisishia Wananchi kuzitumia bila ya usumbufu.
katika Ziara hiyo, Dkt. Khalid ametembelea Barabara ya Mchangamle ambayo Ujenzi wake umekamilika, na Barabara ya Tunguu Charawe - Ukongoroni Bwejuu, yenye Urefu wa Kilomita 23.3, ambayo ipo katika hatua za mwisho kukamilika.
Akitoa shukurani kwa niaba ya Wananchi wa Charawe na Ukongoroni Iddi Mkanga Mwita ameipongeza Serikali kwa kuweza kuwatatulia tatizo la Barabara