Jeshi la Polisi nchini limetoa onyo kwa baadhi ya wananchi ambao wamekuwa na tabia ya kukimbilia katika maeneo zinapotokea ajali huku wakiwa na lengo la kuwaibia waathirika wa ajali hizo na wakati mwingine kufanya uharibifu.
Akitoa taarifa hiyo Msemaji wa Jeshi la Polisi,Nchini Naibu Kamishna wa Polisi DCP David Misime amesema jamii inapaswa kuachana na tabia na vitendo hivyo ambavyo ni hatarishi kwa maisha na mali ambazo zimekuwa zikihusika katika ajali hizo.
Misime amesema pamoja na kuwepo kwa kumbukumbu za watanzania kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa vibaya mwaka 2019 Mkoani Morogoro na ajali ya Aprili 14, 2024 eneo la Misugusugu wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani bado baadhi ya wananchi hawajajifunza kutokana na madhara yaliyotokea.
Aidha amewataka Wananchi kutambua kuwa gari lililobeba mafuta ya dizeli na petrol linapopata ajali kwa kiwango kikubwa kunakuwepo na uwezekano wa kutokea mlipuko wa moto, hivyo waendelee kuchukua tahadhari kubwa.
WANAOKIMBILIA MAENEO YA AJALI KWA LENGO LA KUIBA WAPEWA ONYO KALI
stories
standard