Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea kuithamini Kada ya Maabara kuwa ni eneo muhimu la kusaidia uchunguzi wa Maradhi mbalimbali , hivyo imeahidi kuimarisha maslahi ya Wataalamu wa Kada hiyo.
Hiyo ni kauli ya Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi katika Hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Afya Mhe. Nassor Ahmed Mazrui katika Kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Maabara Duniani, ambapo amesema wakati Serikali ilipofanya Maamuzi ya kushiririkiana na Sekta Binafsi katika huduma za Afya ikiwemo Maabara ni kuharakisha ufanisi wa huduma huku ikiendelea kuthamini Wataalamu wa Ndani.
Washirika wa Maendeleo ambao ni AICAP(icap) Tanzania na CDC, wameelezea namna wanavyoshirikiana na Serikali katika kusaidia miradi mbalimbali ya Afya.
Kwa niaba ya Wataalamu wa Mabaara, Ussi Hamza Ussi amesema Kada hiyo imeendelea kuimarika kwa kuwezesha baadhi ya Maabara Nchini kuweza kutambulika Kimataifa.
Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Afya Dkt.Amour Suleiman Mohamed ameshawishi kufanyike ubunifu zaidi pamoja na uwekezaji wa kimaabara ili kuimarisha Afya za Watu.
Maadhimisho hayo yameenda pamoja na Uzinduzi wa muongozo wa Sera ya Maabara za Afya Zanzibar.