Mke wa Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazaaza la Mapinduzi Mama Maryam Mwinyi amewasisitiza Wanawake kusimama imara katika Nafasi zao na kujiamini katika kufanya Maswala mbali ya kimaendeleo na kushiriki katika fursa zinazotokeya Nchini.
Akizungumza wakati akikabidhi Majiko ya Gesi kwa Wanawake Wajasiriamali na Wenye Mahitaji Maalumu huko Maisara ikiwa ni Siku ya Kwanza ya Mwanamke Shujaa. kwa kushirikiana na Kampuni na Mashirika ya Kiserikali na Binafsi Amesema hatua hiyo itawasaidia katika kurahisha kazi zao ikiwemo kuongeza nguvu na ufanisi katika kutekeleza Biashara zao pamoja kujileteya mafanikio ya kimaendeleo.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Watoto Mhe.Riziki Pembe Juma ameeleza kuwa wana malengo ya kuwasaidia Wajasiriamali hasa Wanawake na kuwawezesha katika Nyanja tofauti zitakazomkombowa kimaisha ili kufikiya malengo yao waliokuyakusudia
Wadhamini waliojitoleya katika kutowa Majiko kwa Wanawake Wajasiria mali hao Meneja Mkuu wa Oryx Gass Zanzibar Shuwekha Omari Khamisi na Mkurugenzi Mtendaji kutoka Shirika la Utangazaji ZBC Ndg.Ramadhan Bukini wamesema matarajio yao ni kuhakikisha wanaendeleza mashirikiano ili kuwasaidiya Wanawake kujikwamuwa kiuchumi na kuondokana na utegemezi katika Jamii
Jumla ya Majiko Mia Tatu na Arubaini yaliotelewa kwa Wajasiriamali hao.