POLISI NCHI 14 KUFANYA MAFUNZO KUKABILIANA NA UHALIFU

Jeshi la polisi

      Jeshi la Polisi Nchini linatalajia kuwa, Mwenyeji wa Mafunzo ya utayari kwa vitendo Mwaka huu yatakayo jumuisha Nchi 14 Wanachama wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi ukanda wa Mashariki mwa Afrika  Eeapcco April 13 Hadi 18.

    Akitoa Tarifa Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini Naibu Kamishna wa Polisi David Misime amesema  Mafunzo hayo yanatarajiwa kufanyika katika Shule ya Polisi Tanzania Moshi ambapo  Maafisa, Wakaguzi na Askari wa Vyeo mbalimbali Wapatao 670 wanatarajiwa kushiriki.

     Naibu Kamishna  Misime amebainisha kuwa kufanyika kwa Mafunzo hayo kunatokana na maazimio yaliyofikiwa na Wakuu wa Shirikisho la Polisi Ukanda wa Mashariki mwa Afrika katika Mikutano yao ya kila Mwaka. 

    Amesema kuwa katika Mkutano uliofanyika  Oktoba, 2021 Kinshasa Nchini Congo, Wakuu hao wa Polisi walipitisha Azimio la Zoezi hili kufanyika Tanzania na amezitaja baadhi ya Nchi zinazotarajiwa kushiriki kuwa ni  Mwenyeji Tanzania, Burundi, Eritrea, Djibouti, DRC Congo, Kenya, Comoro, Ethiopia, Shelisheli, Rwanda, Somalia, Sudan, Sudani Kusini na Uganda.

    Msemaji wa Jeshi hilo amebainisha kuwa lengo la Mafunzo hayo na  Mazoezi mengine yaliyopita ni kuwajengea Maafisa, Wakaguzi na Askari wa Vyeo mbalimbali uwezo wa kubaini, kuzuia na kutanzua uhalifu unaovuka mipaka ikiwemo ugaidi, usafirishaji haramu wa Binadamu, Biashara Haramu ya Dawa za Kulevya pamoja na kubadilishana uzoefu na Taarifa za Kitelejensia.

 

 

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.