TULIA TRUST YAREJESHA FURAHA KWA MJANE MBEYA

dkt.Tulia Trust Msaada

 

   Taasisi ya  Tulia Ttrust imetoa msaada wa kumjengea Nyumba ya kuishi Mama Mjane  Singwava Jackson kwa lengo la  kumpunguzia shida na Familia yake.

    Akikabidhi Nyumba hiyo Mwenyekiti wa Taasisi ya Tulia Trust Dkt. Tulia Ackson  amesema Taasisi yake itaendelea kusaidia Jamii hasa Watu wenye mazingira magumu

    Dkt. Tulia  ambae ni Mbunge wa Mbeya Mjini na Spika wa Bunge la Tanzania  amemkabidhi Fedha  Taslim kuanza  mtaji wa kuendeleza maisha yeye na Familia yake ya Watoto Sita Amesema mpango huo utasaidia kuwaondolea shida Wananchi wake pamoja na kuwarahisishia  mazingira ya Maisha yao.

   Akitoa Shukrani zake  Singwava Jackson Mjane mwenye Watoto Sita Mkaazi wa Kata ya Iganjo Jijini Mbeya amesema kuwa kwa kipindi kirefu amekuwa akipambana na kuwaendeleza Watoto wake katika mazingira magumu.

   Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Beno Malisa  kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa  amempongeza Dkt.  Tulia kwa kugusa Maisha ya Watu wenye uhitaji.

    Baadhi ya Majirani waliohudhuria hafla hiyo wamesema kuwa Mama huyo anastahili kusaidiwa kutokana na  mazingira magumu anayoishi..

    Awali kabla ya kukabidhiwa Nyumba Bi Singwava Jackson alikuwa  anajishughilisha na kulea Familia kwa kazi ya kuokota Makopo na anaishi kwenye Nyumba aliyojenga kwa Maturubai kwa Takribani Miaka Miwili.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.