Mke wa Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mariam Mwinyi amevitembelea Vituo vya kulelea Watoto Yatima pamoja na Nyumba za Wazee wasio jiweza kwa kuwapa sadaka ya Eid Fitri.
Akizungumza na Watoto hao Mama Mariam Mwinyi ambae pia ni Mwenyekiti wa Maisha bora Foundation amesema katika kuwajali Watoto Kivitendo Serikali imekuwa nao Karibu kuhakikisha wanasherehekea Sikukuu kwa Utulivu na kuwataka Watoto hao kuendeleza Maadili mema waliojifunza kipindi cha Mwenzi wa Ramadhani.
Aidha amewatembelea na Wazee kwa kuwafariji na kuwaombea Dua kuwa na Afya njema.
Wakitoa Neno la Shukurani kwa Niaba ya Vituo hivyo wasimamizi wa wameishukuru Serikali kwa kuwajali katika kipini chote cha Ramadhani na Sikukuu pamoja na kuwatakia Khery Viongozi kuzidi kuendeleza Majukumu yao ya kuleta Maendeleo ya Nchi.
Katika Ziara hiyo Mama Mariam Mwinyi ameongozana na Viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto n kuvitembelea mbalimbali ikiwemo Kituo cha Kulele Watoto Yatima mambo sasa, SOS, Mazizini nyumba za Wazee Welezo na Sebleni.