MPANGO WA MAGEUZI WA SEKTA YA ANGA

DKT KHALID SALUM MOHAMED

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Dk Khalid Salum Mohammed amesema kupitia mpango wa mageuzi ya Sekta ya Anga Serikali imeweza kupata mafanikio makubwa ya kiuchumi kufuatia kuimarika kwa huduma muhimu kwa Abiria

Akitoa Taarifa kwa Vyombo vya Habari kuhusiana na maendeleo ya Sekta ya Anga Nchini amesema mabadiliko hayo yanayotokana na mipango imara ya Serikali yanayolenga kukuza uchumi kupitia utowaji huduma bora zinazokwenda na wakati na kusababisha kupata tunzo ya uwanja bora barani Afrika

Akizungumzia kuhusiana na utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Dk Khalid amesema wanaendelea kuimarisha Miundombinu ya huduma za usafiri ikiwemo Jengo jipya la Abiria ,Kituo cha Biashara ,Ujenzi wa Vituo vipya vya kutoa huduma za Mafuta ya Ndege na Mradi wa eneo la kuhifadhia na kusafirishia Mizigo ya Chakula

Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Seif Abdallah Juma amesema wamefanikiwa kuimarisha ulinzi hasa katika uingiaji Dawa za Kulevya ,pamoja na kuimarisha mfumo bora wa kuhudumia Abiria kupitia idara ya Uhamiaji

Wakati huo huo Waziri Dk Khalid alifanya Ziara ya kutembelea baadhi ya maeneo ya Ujenzi wa Miradi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.