Mamlaka ya udhibiti wa huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA), imetangaza Bei mpya za Mafuta ambapo Mafuta ya Petrol, Disel na Mafuta ya Ndege yameendelea kupanda kwa Mwezi huu.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa Habari katika Ofisi ya Mamlaka hiyo Maisara Meneja kitengo cha Mahusiano Mbaraka Hassan Haji, amesema Bei ya Mafuta ya Petrol kwa Mwezi huu itakuwa ni Shilingi 3,133 kutoka Shilingi 3,118 ya Mwezi uliopita.
Aidha Mbaraka amefahamisha kuwa ZURA inapanga Bei kwa kuzingatia mambo mbalimbali ikiwemo wastani wa mwenendo wa mabadiliko ya Bei za Mafuta Duniani, gharama za uingizaji mafuta katika Bandari ya Dar es salam na Tanga na gharama za mabadiliko ya fedha za Kigeni zinazotumika kununulia Mafuta
stories
standard